


Kongamano la Kimataifa
la 11 la
Kauli Mbiu 2026
Twen’zetu Makerere! Lulu ya Afrika Yaita. Upo?
CHAUKIDU2026
"Kiswahili na Lugha Nyingine Afrika: Mustakabali wa Ndani na Nje ya Mipaka ya Darasa katika Dunia Inayobadilika"


Chuo Kikuu cha
Makerere
Ungana nasi katika kitovu cha elimu cha Afrika Mashariki. Makerere inatoa mazingira ya kipekee ya kitaaluma kwa ajili ya mjadala mpana kuhusu mustakabali wa lugha ya Kiswahili duniani.
Kutana na wataalamu, wakereketwa, na wadau wa Kiswahili toka sehemu mbalimbali Duniani.
Utafurahi kutangamana na Waswahili wengine na kuwa sehemu ya familia kubwa ya wasemaji wa Kiswahili Duniani! Mada kuu ni “Kiswahili na Lugha Nyingine Afrika: Mustakabali wa Ndani na Nje ya Mipaka ya Darasa katika Dunia Inayobadilika.” Jioni ya tarehe 12 Disemba, kutakuwa na tamasha kubwa la Utamaduni wa Mswahili, ambapo watu wote wanakaribishwa, hata wale ambao hawakushiriki katika kongamano.
Kamati ya maandalizi inaangalia uwezekano wa kuandaa shughuli za kitalii. Wale watakaohitaji kushiriki katika utalii watajulishwa gharama zitakuwa kiasi gani na ni maeneo gani ya kiutalii yatakayotembelewa.

"Kiswahili na Lugha Nyingine Afrika: Mustakabali wa Ndani na Nje ya Mipaka ya Darasa katika Dunia Inayobadilika."
Mikondo ya Mazungumzo
Nafasi ya Kiswahili na Lugha Nyingine Afrika na Kwingineko katika Ushindani wa Kimataifa.
Matumizi ya Kiswahili katika Jamii: Nyumbani, Kazini, Biashara na Huduma za Kijamii.
Vyombo vya Habari, Mitandao ya Kijamii, na Maudhui ya Dijitali katika Kupanua Matumizi ya Kiswahili.
Vijana, Ubunifu, na Mabadiliko ya Kiswahili.
Kiswahili na Lugha nyingine: Ushirikiano, Ushindani, na Mustakabali wake.
Nafasi ya Kiswahili katika Sera na Utawala wa Lugha Barani Afrika na Kimataifa: Mchango na haja ya kuwa na Asasi za Kiswahili.
Kiswahili kama Nyenzo ya Uchumi na Ujasiriamali.
Ufundishaji wa Kiswahili Ndani na Nje ya Mfumo Rasmi wa Elimu: Fursa na Changamoto.
Kiswahili na Diaspora: Utambulisho, Uhamiaji, na Urithi wa Lugha.
Kiswahili katika Sanaa, Tafsiri, na Ukalimani: Fasihi, Muziki, Filamu, na Mawasiliano ya Lugha.
Tenga Tarehe Hii
- Hatua 13 Juni 2026Mwito wa Ikisiri
- Hatua 220 Julai 2026Makataa ya Mwito wa Ikisiri
- Hatua 330 Septemba 2026Taarifa ya Kukubaliwa
- Hatua 431 Oktoba 2026Mwisho wa Usajili wa Mapema
- Hatua 510–13 Disemba 2026Kongamano katika Chuo Kikuu cha Makerere
Sauti za Kitaaluma.






Karibu Kampala. Karibu CHAUKIDU.
Jiunge na jumuiya ya kimataifa iliyojitolea kwa mustakabali wa Kiswahili na lugha za Kiafrika.