Showing the single result
Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika katika Zama za AI: Fursa na Changamoto
December 14, 2025
- December 16, 2025
9:00 am
- 10:00 pm
Chuo Kikuu cha Kibabii, Bungoma, Kenya
Katika zama hizi za Akili Mnemba/Akili Unde (Artificial Intelligence – AI), ambapo teknolojia hii inaendelea kubadilisha kila nyanja ya maisha ya binadamu, uga wa lugha haujaachwa nyuma. CHAUKIDU inafikiri ni vyema kuwa na mjadala wa kina katika suala hili, na kongamano letu la Kimataifa ndilo litupalo uwanja mpana wa kufanya hivyo kwa mafanikio makubwa. Wanachama wa CHAUKIDU na wadau wote wa Kiswahili na teknolojia wanakaribishwa kutuma ikisiri za makala zinazochambua ama kujadili suala hili katika kongamano la 10 la Kimataifa la CHAUKIDU. Wanaweza kutuma ikisiri za makala kuhusu mada kuu ya Kongamano huku wakimakinikia mada ndogondogo zifuatazo: