Twende Bungoma 2025

Kongamano la Kimataifa la CHAUKIDU

Kongamano la Kimataifa

Chaukidu huandaa kongamano hili la mwaka la kimataifa katika mwezi wa Disemba ili kuwakutanisha wataalamu, wakereketwa, na wadau wa Kiswahili toka sehemu mbalimbali Duniani. Kongamano hili ni tofauti na lile la mwaka lifanyikalo mwezi wa Aprili sambamba na Kongamano la Mwaka la Chama cha Walimu wa Lugha za Kiafrika (African Language Teachers Association – ALTA). Mada za makongamano ya kimataifa zinakuwa ni zile zigusazo mawanda mapana ya lugha ya Kiswahili. Hadi sasa, CHAUKIDU imekuwa na makongamano saba ya kimataifa ambayo ni Kongamano la Washington DC (2015), Kongamano la Nairobi (2016), Kongamano la Dar es Salaam (2017), Kongamano la Unguja (2018), Kongamano la Kampala (2019), Kongamano la Kilifi (2021), na Kongamano la Washington, DC (2022).

Watoa Mada-Elekezi

Tutakuwa na watoa mada elekezi wazuri watakaoamsha mijadala mikali kongamanoni.

Uwasilishaji wa Makala

Unaruhusiwa kuwasilisha makala yako kongamanoni. Ili uweze kuwasilisha makala, tafadhali tuma ikisiri yako. Ikisiri hiyo itafanyiwa tathmini kabla ya kupewa nafasi ya kuiwasilisha kongamanoni.

Kwanini ushiriki kongamanoni?

Ni kwanini Ushiriki?

Yawezekana unajiuliza swali hili: ni kwanini nishiriki kwenye kongamano hili? Nitapata faida gani?

Ujumuikaji

Kongamano la Kimataifa la CHAUKIDU linakuwa fursa ya kujumuika katika harakati za kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili

Wasemaji Mahiri

Kongamano hili litakupa fursa ya kusikiliza mawasilisho ya mada elekezi kutoka kwa wasemaji mahiri na waliobobea katika fani zao.

Pata Marafiki Wapya

Kongamano hili linakupa fursa ya kukutana na watu mbalimbali toka sehemu mbalimbali za dunia. Kutana na watu wapya kongamanoni!

Tukakongamaneni

Kuhusu Kongamano Hili

Kuhusu Kongamano Hili

Kutana na wataalamu, wakereketwa, na wadau wa Kiswahili toka sehemu mbalimbali Duniani. Utafurahi kutangamana na Waswahili wengine na kuwa sehemu ya familia kubwa ya wasemaji wa Kiswahili Duniani! Mada kuu ni Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika katika Zama za AI: Fursa na Changamoto. Jioni ya tarehe 16 Disemba, kutakuwa na tamasha kubwa la Utamaduni wa Mswahili, ambapo watu wote wanakaribishwa, hata wale ambao hawakushiriki katika kongamano.

Kamati ya maandalizi inaangalia uwezekano wa kuandaa shughuli za kitalii. Wale watakaohitaji kushiriki katika utalii watajulishwa gharama zitakuwa kiasi gani na ni maeneo gani ya kiutalii yatakayotembelewa.

Jiwekee Nafasi

Harakisha! Watakaojisajili mapema watapata punguzo!

Wale watakaojisajili mapema, watalipa ada yenye punguzo. Pia, ukiwa mwanachama hai wa CHAUKIDU kwa mwaka huu, unapata punguzo zaidi.

Ada ya Kongamano

Lipia Kongamano

Usichelewe. Lipa ada yako ya kongamano sasa.

Gold

Basic Package

$ 39 00 / person
  • Gold row seat
  • Snack and drinks
  • Event Mechandise

Diamond

Pro Package

$ 89 00 / person
  • Gold row seat
  • Snack and drinks
  • Event Mechandise

Platinum

Enterprise Package

$ 129 00 / person
  • Gold row seat
  • Snack and drinks
  • Event Mechandise
0 +
Wawasilishaji
0 +
Washiriki
0
Siku za Kongamano
0 +
Saa za Kongamano

Wadhamini Wetu

Wadhamini

Kongamano haliwezi kufanikiwa bila kuwa na wadhamini. Ikiwa ungependa kuwa mdhamini wa kongamano la CHAUKIDU, tuandikie nasi tutaweka nembo ya taasisi au biashara yako hapa katika tovuti yetu na kwenye vitabu vyetu vya kongamano.

Wadhamini Wakuu
Wadhamini Wengine
Vyombo vya Habari

Shuhudia Kongamano Kubwa la Kiswahili Nchini Kenya Tena

Hii ni nafasi kwa Watanzania, WanaAfrika Mashariki, na wadau wa Kiswahili kote duniani kufika katika mji wa Bungoma na kuwa sehemu ya kongamano hili kubwa.