Mpenzi mdau wa Kiswahili,
Tunayo furaha kukuletea mwaliko huu wa kujiunga na jumuiya ya Chaukidu, chama kisichokuwa na malengo ya kupata faida za kifedha. Kama mmoja wa watu wenye (au watarajiao kuwa na) mahusiano na Afrika ya Mashariki, lugha ya Kiswahili na utamaduni wake, tunaamini jumuiya hii itakunufaisha. Vilevile tunaamini kuwa utaifaidisha pia jumuiya hii kwa mawazo yako na uanachama wako. Kwa hiyo, uanachama wako utakuwa ni hatua muhimu sana ya kutuwezesha kufikia moja ya malengo yetu – kuwapa watu wote duniani fursa ya kujiunga na jumuiya yenye umuhimu mkubwa.
Ada yetu kwa wanachama wapya kutoka katika dayaspora (wale waishio nje ya Afrika Mashariki) ni kidogo tu – $30 kwa uanachama wa kawaida, na $15 kwa wanafunzi wasomao katika taasisi mbalimbali katika dayaspora. Uanachama wa kawaida kwa waishio Afrika ya MAshariki ni $20 na kwa wanafunzi waishio Afrika ya Mashariki ni $5 tu.
Kujiunga na chama hiki, tafadhali lipia ada kwa kujaza fomu fupi hapo chini. Unaweza pia kulipia ada yako ya uanachama kwa mwakilishi wa Chaukidu/mjumbe wa bodi aliye karibu nawe. Kama una swali lolote, tafadhali usisite kuwasiliana na Mkurugenzi Mtendaji kupitia secretariat@chaukidu.org. Unaweza pia kujaza fomu iliyoambatishwa hapa na kulipa kwa kutumia Paypal.
Tunayo furaha kuwa tupo hapa kwa ajili yako, na kwamba tutafanya kazi hii kwa pamoja.
Kulipia Ada ya Uanachama kwa Simu
Tunatambua uwepo wa wale ambao hawataweza kulipia ada zao kwa njia ya kadi ya benki ama PayPal. Tumeandaa utaratibu mzuri kwa watu wa nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na wengine walioko nje ya Afrika Mashariki. Tuna wawakilishi maeneo mbalimbali na tumewapa ruhusa ya kukusanya ada kwa njia zifaazo katika nchi husika. Ulipapo ada yako kwa mwakilishi wa CHAUKIDU, ataifikisha kwa Mhazini na utapewa stakabadhi rasmi kwa malipo yako na kuingizwa katika daftari la wanachama wa CHAUKIDU. Ikiwa umelipa ada yako lakini hata baada ya wiki moja hujapata stakabadhi yako, tafadhali wasiliana na yule aliyepokea ada hiyo au uongozi wa CHAUKIDU.