Katika zama hizi za Akili Mnemba/Akili Unde (Artificial Intelligence – AI), ambapo teknolojia hii inaendelea kubadilisha kila nyanja ya maisha ya binadamu, uga wa lugha haujaachwa nyuma. CHAUKIDU inafikiri ni vyema kuwa na mjadala wa kina katika suala hili, na kongamano letu la Kimataifa ndilo litupalo uwanja mpana wa kufanya hivyo kwa mafanikio makubwa. Wanachama wa CHAUKIDU na wadau wote wa Kiswahili na teknolojia wanakaribishwa kutuma ikisiri za makala zinazochambua ama kujadili suala hili katika kongamano la 10 la Kimataifa la CHAUKIDU. Wanaweza kutuma ikisiri za makala kuhusu mada kuu ya Kongamano huku wakimakinikia mada ndogondogo zifuatazo:
Wasemaji Wakuu
Taarifa za wasemaji wakuu (watoa mada-elekezi) wa CHAUKIDU Arusha 2023 zitawekwa hapa zitakapokuwa tayari.

Msemaji wa Kwanza
Prof. Jina Jina

Msemaji wa Pili
Prof. Jina Jina

Msemaji wa Tatu
Prof. Jina Jina

Msemaji wa Nne
Prof. Jina Jina
Ungependa kuwa mmoja wa wawasilishaji katika kongamano hili?
Kama jibu lako ni ‘ndiyo’ basi tutumie ikisiri yako sasa. Taarifa na zaidi na mwito wa ikisiri zinapatikana kwa kubofya kitufe kilichopo hapo chini.