Kongamano la Kimataifa la CHAUKIDU
Kongamano la Kimataifa
Chaukidu huandaa kongamano hili la mwaka la kimataifa katika mwezi wa Disemba ili kuwakutanisha wataalamu, wakereketwa, na wadau wa Kiswahili toka sehemu mbalimbali Duniani. Kongamano hili ni tofauti na lile la mwaka lifanyikalo mwezi wa Aprili sambamba na Kongamano la Mwaka la Chama cha Walimu wa Lugha za Kiafrika (African Language Teachers Association – ALTA). Mada za makongamano ya kimataifa zinakuwa ni zile zigusazo mawanda mapana ya lugha ya Kiswahili. Hadi sasa, CHAUKIDU imekuwa na makongamano saba ya kimataifa ambayo ni Kongamano la Washington DC (2015), Kongamano la Nairobi (2016), Kongamano la Dar es Salaam (2017), Kongamano la Unguja (2018), Kongamano la Kampala (2019), Kongamano la Kilifi (2021), na Kongamano la Washington, DC (2022).
Watoa Mada-Elekezi
Tutakuwa na watoa mada elekezi wazuri watakaoamsha mijadala mikali kongamanoni.
Uwasilishaji wa Makala
Unaruhusiwa kuwasilisha makala yako kongamanoni. Ili uweze kuwasilisha makala, tafadhali tuma ikisiri yako. Ikisiri hiyo itafanyiwa tathmini kabla ya kupewa nafasi ya kuiwasilisha kongamanoni.
